Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi yapokea miradi ya uwajibikaji kwa jamii CSR inayogharimu jumla ya shilingi milioni 490.9 kutoka kampuni ya Shanta Mgodi wa Singida mwaka wa fedha 2022/2023.
Ziara hiyo ya kutembelea, kukagua na kupokea miradi hiyo imeanza hii leo tarehe 02 Juni, 2025 katika Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida ambapo kamati hiyo imetembelea miradi 10 ili kujiridhisha kuhusu ubora na ukamilifu wa miradi hiyo.
Kamati imepokea Trekta na Tela yake yenye thamani ya shilingi milioni 85.5, vitanda vya dabo deka magodoro na blanketi shule ya msingi Ikungi kwa watoto wenye mahitaji maalumu vyenye thamani ya shilingi milioni 12.5, matundu 20 ya vyoo yenye thamani ya shilingi 47.3 pamoja na madawati 300 yenye thamani ya shilingi 32.5 shule ya msingi Mwau, madara mawili na ofisi yenye thamani ya shilingi milioni 62.5 pamoja na matundi tisa ya vyoo yenye thamani ya shilingi milioni 24.2 na mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 41.8 katika shule ya msingi Mbogho,
Vile vile kamati imefika mradi wa ujenzi wa zahanati kijiji cha Mang'onyi unaogharimu takribani shilingi milioni 159.5, ujenzi wa barabara ya vumbi kilomita 6 yenye kugharimu milioni 12.5, pamoja na mradi wa ukarabati na zahanati kijiji cha Sambaru unaogharimu shilingi milioni 12.5
Katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe. Ally J. Mwanga kwa niaba ya wanachi na madiwani ametoa shukrani kwa miradi hiyo ya CSR kwani imekuwa msaada kwa wananchi wilayani Ikungi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Kastory Msigala amesisitiza kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati na kwa ubora kwa kuzingatia ushauri wa Wahandishi na Maafisa Manunuzi ili kutengeneza miradi bora wilayani hapa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa