Mwenyekiti wa Halamashauri ya Wilaya ya Ikungi Mhe Ally J.Mwanga aweka jiwe la msingi katika soko kuu jipya kijiji cha Ikungi.
Akizungumza kabla ya kuzindua mradi huo tarehe 10 februari 2023 amesema kuwa wajasiriamali wamepata eneo zuri kwa ajili ya kuuza mbogamboga matunda pamoja na bidhaa za nafaka kwa uhuru tofauti na mazingira ya mwanzo ambapo wafanyabiashara wa eneo hilo walivyokuwa wakiteseke maeneo ya kuuzuia bidhaa zao.
Aidha amewataka wafanyabiashara hao kutunza mazingira yanayozunguka soko hilo pamojan na ndani ya soko ili kulifanya soko hilo liwe la kudumu zaidi.
Soko hili limejengwa na shirika la TAHA kwa kushirikiana na UN Women kupitia ufadhili wa KOICA kwa ajili ya kuboresha huduma za masoko kwa wakulima wa wilaya ya Ikungi.
kwa upande wao wafanyabiasahara wa eneo hilo wameshukuru kwa kujengwa kwa soko hilo kwani mwanzoni walipata adha ya kunyeshewa mvua kuibiwa bidhaa zao na hali ya usafi kwa sasa wamepata eneo lenye ulinnzi na ni safi kwa kuuzia bidhaa zao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa