Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wafanya kikao na waganga wafawithi katika Wilaya ya Ikungi kujadili changamoto ya huduma za wazee na watoto juu ya upataji wa huduma za afya.
Katika kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 15 Juanuari 2025 ukumbi wa Halmashauri viongozi kutoka taasisi hiyo wamesema tafiti zimefanywa na taasisi hiyo kujua hali ya utoaji huduma za afya kwa watoto na wazee hivyo wamekaa kujadili juu ya miongozo iliyotolewa na serikali kuhusu msamaha huo upande wa afya.
Kwa upande wao waganga wafawidhi wakati wa mjadala huo wametoa maoni yao kuwa ni pamoja na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa wazazi wenye watoto pamoja na wazee hivyo kupelekea kukosa haki zao za msingi.
Wajumbe wa kikao hicho pia wameongeza na kusema kuwa uchache wa wahudumu pamoja na uchache wa vifaa tiba imekua changamoto.
"Pia kumekua na muingilino wa maswala ya kisiasa katika utoaji wa huduma hizo."wamezungumza wafawidhi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa