Makamu mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora Mhe. Mohamed Hamis Hamad akiongozana na timu yake afika kutoa elimu ya haki za binadamu kwa wananchi na watendaji wa kijiji cha Mahambe kata ya Unyahati na, shule ya sekondari Ikungi.
Wakitoa elimu hiyo katika shule ya sekondari Ikungi viongozi hao walitoa elimu ya haki na wajibu wa watoto wakiwa shuleni na majumbani kwao Mwenyekiti amesema kuwa haki hizo ni pamoja na kusoma, kulindwa, kupendwa, kuishi, malazi, mavazi, kutokubaguliwa na kupata huduma za afya.
Hata hivyo wameeleza wajibu wa moto akiwa nyumbani au shuleni kama vile kusaidia wazazi kazi za nyumbani, kuwaheshimu wakubwa, usawa wao kwa wao , uadilifu, uaminifu,ushirikishwaji, maridhiano, na utawala bora ili kulinda amani katiika nchi yetu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa