Kamati Tendaji ya ukaguzi wa bei elekezi ya sukari katika Wilaya ya Ikungi yatembelea katika Vijiji vya Puma,Ikungi,Issuna,Pamoja na Mkiwa katika maduka ya rejareja na jumla kukagua uwepo wa sukari na bei elekezi za serikali kama zinafuatwa ipasavyo,Zoezi hilo limeanza jumatatu ya tarehe 22 Januari mwaka 2024 na litakuwa endelevu mpaka pale kamati itakapojiridhisha kuwa bei elekezi imefwatwa na wauzaji wa maduka hayo Akizungumza na Waandishi wa habari Afisa Biashara Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bwana Robert Augustino Mhokole Amesema Kuna Tangazo la serikali namba 40B la Amri ya bei elekezi ya sukari lililotengenezwa chini ya aya ya 3(2) linaelekeza kiwango Cha juu Cha bei ya sukari mauzo ya jumla na rejareja Tanzania bara hususani maeneo ya ukanda wa kati Dodoma,Singida na Tabora ni shilingi 2,650-2,800 bei za jumla na 2,800-3,000 pekee Kwa bei za rejareja."Lengo ni kutomkandamiza mwananchi wa kawaida kwani wengi wao wapo katika kipindi Cha kilimo hivyo ni muda anaohitaji kujijenga kiuchumi."amezungumza kiongozi huyo kutoka Halmashauri ya IkungiAidha kamati hiyo imewataka wamiliki wa maduka ya jumla na rejareja kutokuificha sukari hiyo Kwa kisingizio kuwa imekuwa adimu Kwa madhumuni ya kupandisha bei inapotokea upungufu wa sukari maeneo hayo."Hatutasita kuwachukulia hatua za kisheria watu wanamna hiyo kwani sio sahihi"Alizungumza Mmoja wa kamati hiyoBaadhi ya wafanya Biashara wamekubali kuiunga mkono serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuifikia adhima ya Amri hiyo iliyotolewa kisheria.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa