Mheshimiwa Mtaturu azindua usajili wa watoto chini ya miaka mitano Wilayani Ikungi
Posted on: March 18th, 2019
Mpango wa kusajili watoto walio chini ya Miaka mitano kuzinduliwa Wilayani Ikungi.
Zoezi la kupatiwa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano kuzinduliwa Ikungi tarehe 15/03/2014 Katika Kituo cha Afya Ihanja. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Ndg, Miraji Mtaturu alizindua zoezi hilo la uandikishaji wa watoto chini ya miaka mitano. Zoezi hili limesimamiwa na Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA) chini ya udhamini wa Shirika la kimataifa UNICEF ambapo watoto chini umri wa miaka mitano watapatiwa vyeti bure pasipo gharama yeyote. Aidha Mtaturu alisema kuwa Serikali inawajali wananchi kwa kuwasogezea huduma ya uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa mahali walipo. Alisema kuwa mwanzoni wananchi walilazimika kufuata huduma Wilayani jambo ambalo lilikuwa linagharimu pesa na muda hasa wa wakazi walio mbali na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya. Hivyo aliwaasa wananchi kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha zoezi hili
Muuguzi wa Kituo cha Afya Ihanja akitoa huduma ya Uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa wananchi waliokuja kuandikisha vyeti vya watoto chini ya umri wa miaka mitano
Baadhi ya wazazi waliofika kituoni hapo kuchukua vyeti vya kuzaliwa wakionesha furaha kubwa kwa kupata vyeti vya kuzaliwa vya watoto pasipo gharama yeyote
Mtoto chini ya umri wa miaka mitano akionesha cheti chake cha kuzaliwa