|
Halmashauri ya wilaya ya IKUNGI mkoani SINGIDA imetekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN MAGUFULI lililotaka viongozi wa wilaya na mikoa kugawa haraka pikipiki zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya Maafisa Elimu wa kata kama hatua ya kusaidia maafisa hao kutekeleza majukumu yao ya kuboresha elimu katika maeneo yao.
Akizungumza katika halfa ya kukabidhi pikipiki 28 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 80 kwa maafisa elimu wa kata, Mkuu wa wilaya ya IKUNGI MIRAJI MTATURU amewataka maafisa hao kuzitunza vizuri pikipiki hizo na hatasita kuchukua hatua kwa maafisa elimu hao ambao watatumia pikipiki katika shughuli zao binafsi.
Mtaturu amesema kilichobaki ni kuja kufanya tathimini baada ya kuwakabidhi maafisa hao pikipiki.
|
. |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mh Juma Ali Mwanga akisisitiza jambo kabla ya ugawaji wa Pikipiki. |
Mgeni Rasimi Mkuu wa wilaya ya Ikungi Miraji Mtaturu. |
Zoezi la uwekaji wa sahihi kwenye mikataba ya ugawaji pikipiki likifanyika baina ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ikungi na mmoja wa waratibu elimu kata. |
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa