Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wampongeza Ndugu Justice Kijazi kwa kuaminiwa kwa mara nyingine na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi baada ya kufanya kazi katika Halmashauri hii kwa kipindi Cha Miaka 6.Wakizungumza Baadhi ya Watumishi katika hafla fupi waliyoiandaa kwa ajili ya kumpongeza Mkurugenzi huyo Bi Agnes Yunge,Ndg Ngwano Ngwano pamoja na Bi Haika Massawe wamempongeza na kusema kwa niaba ya Watumishi wengine na kusema kuwa wapo tayari kushirikiana katika Kila hatua kuhakikisha maendeleo yanakuja kwa Kasi katika Wilaya hiiMkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa upande wake alipopata nafasi ya kuzungumza amesema Anamshuru Dkt Samia Suluhu Kwa Kumwamini na atashirikiana naye bega kwa bega kuhakikisha maendeleo yanakuja Wilaya ya IkungiNdg Kijazi ameongeza na kusema kuwa anavipaumbele vinne katika msimu wake mpya na vipaumbele hivyo ni pamoja na Ukusanyaji mkubwa wa Mapato ya Halmashauri,kujikita katika Kilimo kwa sababu Kuna ardhi ya kutosha,Kutatua migogoro mbalimbali ya Ardhi pamoja na Kutafuta wawekezaji ambao pia watakuwa chachu ya maendeleo Katika Wilaya hii."Naomba sana tushirikiane kama ambavyo tumeshirikiana toka mwanzo ili tuweze kuisogeza Ikungi kimaendeleo"
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa