Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya habari Mhe Nape Nnauye amezindua mnara wa mawasiliano wa shirika la mawasiliano nchini TTCL na kutoa maagizo kwa shirika la umeme Tanzania kupitia wakala wa nishati vijijini REA, wakala wa maji vijijini TARURA kupeleka miundombinu wezeshi ili minara iweze kufanya kazi...
Waziri Nape amesema hayo tarehe 11 Januari,2023 mkoani singida wakati wa uzinduzi wa mnara wa shirika hilo katika kijiji cha Misughaa kilichopo Wilaya Ikungi ambapo ameelekeza TANESCO,RUWASA na TARURA kufikisha huduma hizo ili kupunguza gharama za uendeshaji wa minara hiyo.
katika hatua nyingine waziri Nape ameliagiza shirika la mawasilianmo TTCL kushirikiana na kampuni zingine ili kuleta huduma bora zaidi ambazo zinawapa wananchi unafuu na uhuru wakuchagua huduma wanazohitaji.
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Singida Peter Serukamba Pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi wameahidi kusimamia maagizo ya waziri ili kukuza maendelea ya Wilaya ya Ikungi pamoja na mkoa kwa ujumla.
Pia Mkurugenzi Kijazi amewaomba wananchi kuwa waaminifu katika kuitunza miundombinu ya Mawasiliano inayoletwa na mashirika mbalimbali na kutoa taarifa mapema pindi itokeapo hitilafu mbalimbali.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa