Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Margaret Kapolesya akabidhi VISHIKWAMBI zaidi ya 600 kwa walimu wa shule ya msingi lengo ikiwa ni kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika wilaya hiyo kwani vitatumika katika ufundishaji na ujifunzaji.
Akizungumza kabla ya kukabidhi VISHIKWAMBI hivyo tarehe 11 Januari 2023 Kapolesya amesema kuwa vishikwambi hivyo vitagawiwa kwa walimu wote walio kwenye ajira ya kudumu ya serikali."VISHIKWAMBI hivi ni kwa ujifunzaji na ufundishaji tu matumizi mengine kama kupiga picha na kuweka kwenye mitandao ya kijamii hairuhusiwi"alizungumza kapolesya.
Kapolesya ameongeza na kusema kuwa VISHIKWAMBI ni mali ya serikali hivyo mwalimu anapofukuzwa,kuacha kazi,kufariki ama kuhama anapaswa kurudisha kishikwambi hicho katika tasisi husika aliyokabidhiwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa