Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kasim Majaliwa Majaliwa amefanya ziara ya ukaguzi na kisha kuweka mawe ya msingi ya chuo cha mafunzo ya ufundi VETA pamoja na hospital mpya ya wilaya ikungi na kutembelea kituo cha afya Iglanson
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mhe. Muro amesema ziara ya waziri imeleta faraja kwa wananchi wa ikungi kutokana na maelekezo yaliyotolewa na waziri mkuu majaliwa yanayokwenda kukamilisha miradi yote ya maendeleo ikiwemo hospitali mpya ya wilaya na kituo cha afya Iglanson na chuo cha veta ambavyo amevitembelea
Dc Muro amesema kwa upande wao wanajipanga pamoja na uongozi wa halmashauri na veta kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa na Mheshimiwa waziri mkuu majaliwa ndani ya muda mfupi ili wananchi wapate huduma bora za kijamii.
Naye mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Ndugu Justice Kijazi amemshukuru Waziri mkuu kwa Kukubali kuweka mawe ya msingi ya miradi yote mitatu na kuahidiwa kupatiwa watumishi wa kutosha pindi miradi hio itakapokamilika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa