Wilaya ya Ikungi, iliyopo mkoani Singida, ina shughuli za uchimbaji wa madini, hususan dhahabu. Kampuni ya Shanta Mining Company Limited inamiliki na kuendesha Mgodi wa Dhahabu , ambao ulianza rasmi uzalishaji mwanzoni mwa mwaka 2023 baada ya kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu muhimu.
Uwepo wa mgodi mkubwa wa Shanta, meleta fursa mbalimbali za ajira kwa wakazi wa Ikungi na maeneo jirani, pamoja na kuchangia katika miradi ya maendeleo ya jamii. Serikali imehimiza kampuni husika kuhakikisha utekelezaji wa mpango wa uwajibikaji kwa jamii (CSR) na kuzingatia sheria za matumizi ya malighafi za ndani (Local Content) ili kuhakikisha kuwa jamii inayozunguka mgodi inanufaika na uwekezaji huo.
Mbali na mgodi huu mkubwa, wachimbaji wadogo pia huendesha shughuli zao katika maeneo mbalimbalindani ya wilaya.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa