Afisa Elimu Msingi na Awali Bi Margaret Kapolesya ametembelea Shule mpya ya Msingi Ituru Mtavira kukagua maendeleo ya Shule hiyo na kuzungumza na wanafunzi.Kapolesya amezungumza na wanafunzi katika shule hiyo mpya na kusema kuwa namna nzuri ya kusema Asante kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Docta Samia Suluhu Hassan ni wao kusoma kwa bidii na kuyatunza mazingira na majengo hayo yaweze kudumu zaidi kwa vizazi vijavyo pia Aidha amewataka walimu kufundisha kwa bidii ili kubadili matokeo ya wanafunzi Wilaya ya Ikungi na mkoa wa Singida kwa Ujumla."fedha nyingi zinaletwa kwa ajili ya maendeleo sekta ya elimu hatuna budi kubadili matokeo ya wanafunzi na kuwa mazuri zaidi ya mwanzo" Amesema Kapolesya
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa