Afisa kazi Mkoa wa Singida Ndg. Boniphas Michael Mtalula apongeza uendeshaji wa mabaraza ya wafanyakazi katika Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi.
Afisa huyo ambaye amemuwakilisha Kamishna wa kazi mwenye mamlaka ya kusimamia ushirikishwaji wa wafanyakazi mahali pakazi na stahiki za wafanyakazi.
Hayo yamesemwa leo tarehe 08 Februari 2025 mara baada ya kufanyika kikao cha kupitia na kujadili bajeti ya Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi, ambapo amesisitiza mabaraza ya wafanyakazi kujifunza kutoka Wilaya ya Ikungi kwani viongozi wamekuwa wakiwashirikisha vyema wajumbe wa kikako ili kupata maoni ya pande zote juu ya bajeti 2024/2025
Afisa kazi ameomba serikali kusikiliza kwa kina maoni ya wafanyakazi kupitia vikao mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mabaraza ya wafanyakazi pamoja na bajeti kwani ndipo wanapotoa changamoto zao na namna nzuri ya kuboresha mazingira ya wafanyakazi na utendaji wao.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa