Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi leo tarehe 1 agasti 2024 wametembelewa na Amani Girls Organization (AGO)ambayo ni asasi isiyo ya kiserikali kwa lengo la kuimarisha ustawi wa watoto,vijana na wanawake walio katika mazingira hatarishi nchini tanzania ,kwa kuzingatia kukuza maendeleo ya jamii kupitia usawa wa kijinsia Afisa mafunzo Ndg David Fanuel na Sauda Sultan wamesema mradi utatekelezwa na Amani Girls Organization pamoja na Stromme Foundation kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa wilaya ya Ikungi,Iramba na Manyoni.Pia ameongeza kwa kusema mradi utajikita kwenye elimu ya awali,malezi na makuzi ya watoto,uwezeshaji wa vijana wa rika balehe(BONGA) na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi(vikundi vya Vijana kijamii vya kuweka akiba)Amesema shughuli zitakaso tekelezwa ni kuongeza uandikishaji na mahudhurio ya watoto shuleni,upatikanaji wa teknologia rafiki kwa watoto wenye uhitaji maalum,kuboresha miundo mbinu ya shule na vitendea kazi na utawala wa shule na utendaji kazi wake,kuimarisha ujuzina uwezo wa walimukutumia majukwaa mbalimbali ili kuongeza ufahamu katika masuala ya tamaduni mbay,ushirikishwaji wa vijana katika masual ya maendeleo,kuanzisha na kusimamia vikundi vya kuweka akiba,na kukuza vikundi mpaka kuwa asasi za kijamiiMwisho wakuu wa idara na wajumbe wamechangia na kutoa maoni ,ushauri na kupendekeza kata zitakazo pitiwa na mradi huo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa