Askari wa jeshi la akiba 141 wanaume ikiwa ni 121 na wanawake 20 wilaya ya Ikungi wahitimu mafunzo yaliyodumu kwa zaidi ya miezi mitatu katika kata ya Kituntu wilayani hapa.
Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo tarehe 23 Novemba, 2024 mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson amewapongeza wote walioonyesha nidhamu mpaka kufiki siku ya kuhitimisha mafunzo hayo na kuwaomba waende kuwa mabalozi wazuri ili kudumisha amani katika Wilaya hii.
Hata hivyo amempongeza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice L. Kijazi kwa kuonyesha ushiriki wake katika kila yanapotokea mafunzo ya jeshi la akiba kwa kutatua changamoto mbalimbali akishirikiana na madiwani.
Mkuu wa Wilaya amesema kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imekuwa ikitoa kipaumbele kwa waliopata mafunzo ya jeshi la akiba Mgambo kujiunga na jeshi la kujenga taifa na kuwapa fursa mbalimbali zinazojitokeza ndani ya Wilaya na hata kwingineko
Kwa upande wake Kaimu mshauri wa Mgambo Wilaya ya Ikungi amesema kuwa kambi hiyo ilipokea jumla ya wanafunzi 192 wanaume 154 na wanawake 38 na kati yao wanafunzi 42 hawakuendelea na mafunzo baada ya kuchaguliwa kujiunga na Jeshi la kujenga taifa kwa kujitolea na wanafunzi tisa hawakumaliza mafunzo kwa sababu za utoro.
"Wanafunzi hao wamesoma masomo mbalimbali na lengo kuu ni kuwajengea uzalendo, kuwajengea ukakamavu, kudumisha nidhamu na kuwaweka tayari kwa lolote litakalotokea" amezungumza mshauri wa Mgambo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa