katika mwaka wa fedha 2024/2025,halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ilipanga kukusanya na kutumia jumla ya shilingi Bilioni 10.9 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kutoka kerikali kuu, huku wahisani na mapato ya ndani ikiwa ni bilioni 1.2 na mpaka sasa halmashauri imepokea jumla ya Shilingi bilioni 5 ambazo zinaendelea kutumika katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani hapa.
Akisoma taarifa katika baraza la madiwani Wilaya ya Ikungi tarehe 31 Octoba, 2024 ukumbi wa mikutano Halmashari, Mkurugenzi mtendaji Ndg Justice L. Kijazi amesema kuwa katika mwaka wa fedha 2024/2025 halmashauri ya Wilaya ya Ikungi katika bajeti yake ya utekelezaji wa miradi kwa fedha za mapato ya ndani hadi kufikia siku ya kikao hiki imepeleka jumla ya shilingi milioni 440 kutekeleza miradi kama vile Ujenzi wa nyumba 1 ya mwalimu katika shule ya msingi Magungumka, Ujenzi wa Matundu 32 ya vyoo na vyumba 6 vya madarasa katika shule za msingi za Nali, shule shikizi Sanya-Lighwa, Ufana, Mankumbi, Msosa, Shule shikizi Mtakuja-mwaru, Utengenezaji wa madawati ya wanafunzi kwa shule za msingi, Ukamilishaji wa miundombinu ya afya katika zahanati ya Muhintiri, Mwaru, tupendane, mgungira, Choda, Makhonda na vituo vya afya vya Irisya, Iyumbu na ntuntu, pamoja na Ujenzi wa matundu ya vyoo 29 katika shule za sekondari za Ighombwe, Masinda day, Ntuntu, Mang’onyi shanta, Miandi na Muhintiri.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson katika hotuba yake amesema kuwa kuna haja ya halmashauri kubuni vyanzo vya mapato vya kudumu kama vile kuanzisha vituo vya mafuta, vivutio ya kitalii, kuhifadhi misitu ili kuzalisha hewa ya ukaa pamoja na kuanzisha hoteli za kisasa vyanzo ambavyo ni vyakudumu tofauti na baadhi ya vilivyopo ambavyo vinaingiza mapato kwa msimu.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Mhe.Ally J. Mwanga amewataka madiwani kuwa mabalozi wazuri katika ukusanyaji wa mapato wakishirikiana na watendaji wa kata na vijiji pamoja na utunzaji wa misitu kama vile msitu wa Mlilii pamoja na Msitu wa Minyughe kwa maslahi mapana ya Halmashauri yetu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa