Baraza la wafanyakazi wakaa kikao maalumu kujadili rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024
Baadhi ya ajenda zilizojadiliwa hii leo tarehe 06 Februari 2023 ni pamoja na kupitia na kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2022/2023 pia baraza lilijadili makisio ya rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Pia baraza limeipongeza Serikali kwa kujali wafanyakazi kuhakikisha wanalipwa stahiki zao kwa wakati na kuomba kupandishwa madaraja,motisha,na kuwekwa kwa matukio ya kitaifa katika bajeti.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi Ambaye ndiye alikua Mwenyekiti wa kikao hicho amewaomba wafanyakazi kuzingatia maadili kazini na kufuata kanuni na taratibu za kazi.
Na ameagiza kutatuliwa kwa changamoto mbalimbali za wafanyakazi katika wilaya ya Ikungi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa