Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Leo 16 novemba 2023 ,imetembelewa na kaimu meneja wa banki ya Dunia Bi Noreen Beg kwaajili ya ufuatiliji wa miradi ya BOOST NA SEQUIP katika shule za awali ,msingi na Sekondari.Katika ziara hiyo Bi Noreen amekagua mradi wa shule ya sekondari ya Nkuhi Mtaturu iliyopo kata Issuna kiusalama zaidi katika jamii na mazingira yaliyopo shule hiyo ,lengo la mtaalam huyo wa kikanda usalama na mazingira amesema kuwa ni kutoa usaidizi zaidi katika usimamizi wa vihatarishi vya mazingira.Mratibu msaidizi wa SEQUIP kutoka tamisemi ndg Msigwa ameipongeza timu nzima ya wataalam kwa kusimamia vema mradi huo ipasavyo na kusema kuwa wilaya ya Ikungi imefanya vizuri zaidi.Mwisho wananchi wa eneo Hilo wametoa shukrani zao kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Samia Suluhu Hassan na banki ya Dunia kwaajili ya watoto wao kupata shule karibu na itawasaidia kuepuka na vishawishi mbalimbali vilivyokuwa vinawakabili .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa