Zaidi ya Bilioni 1.8 zatumika ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 30 katika barabara ya Mtamaa Minyughe Mtavira yenye urefu wa kilomita 27 katika Wilaya ya Ikungi.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo katika ziara ya kamati ya siasa Mkoa wa Singida tarehe 10 Juni, 2025 katika kijiji cha Minyughe Meneja wa wakala wa barabara za vijijini na mjini Tanzania TARURA Mhandisi Ally Mimbi amesema daraja hilo linaunganisha kata ya Minyughe na Makilawa zenye jumla ya wakazi 26,339.
Mimbi ameongeza na kusema kuwa daraja hilo litawanufaisha wakazi wa maeneo hayo ambao wanajishughulisha na shughuli za kilimo cha biashara na chakula.
“Kupitia daraja hili itasaidia usafirishaji wa mazao ya biashara na chakula pamoja na huduma zingine za kijamii kufikika kwa urahisi” amefafanua Mimbi.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa singida Mheshimiwa Martha Mlata akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego,Waju
mbe wa Kamati ya Siasa Mkoa na Wilaya ya Ikungi, Mkuu wa Wilaya, na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ,wamepongeza ujenzi wa daraja hilo la kisasa la vyuma kwani ilikuwa jikwazo kwa wananchi.
“Daraja hili ni miongoni mwa madaraja bora,makubwa na yakisasa katika Mkoa wa Singida nahimiza miundombinu yake itunzwe ili iweze kudumu zaidi” amezungumza Mhe. Martha Mlata
Naye mwenyeji wa ugeni huo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mheshimiwa Thomas Apson ameshukuru ujio wa Kamati hiyo na kuahidi kushirikiana kwa karibu na tasisi mbalimbali kuhakikisha ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa vyema.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa