Zaidi ya Bilioni 47.4 zinakadiriwa kukusanywa na kutumika katika Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi katika mwaka wa fedha 2025/2026.
Wakizungumza leo tarehe 13 Februari, 2025 katika Kikao maalum cha kamati ya ushauri Wilaya ya Ikungi DCC kujadili rasimu ya mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026, wajumbe wa kikao hicho wamejadili kwa kina rasimu ya bajeti hiyo na kuipitisha kwa lengo la kukuza maendeleo wilayani hapa.
Mkuu Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson wakati wa kikao hicho ameagiza miradi mbalimbali kukamilika kwa wakati pindi fedha za ujenzi wa miradi hiyo kutoka ili miradi hiyo kutumika kuhudumia wananchi.
Akiwasilisha rasimu hiyo Ndg.Juma Msupha kwa niaba ya Afisa Mipango Wilaya ya Ikungi ametaja vipaumbele vya Halmshauri kuwa ni pamoja na kuboresha miundombinu katika mabwawa ya samaki, ukamilishaji wa miundombinu mbalimbali ya ujenzi, kuboresha kilimo, usafi wa mazingira, kuwezesha vikundi kwa kutoa mikopo, kuboresha lishe, ulipaji wa madeni, kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi,
Afisa misitu na uhifadi wa nyuki wilaya ya Ikungi amewasilisha utekelezaji wa mradi wa BEVAC unaofadhiliwa na nchi wanachama wa umoja wa Ulaya na kutekelezwa na shirika la maendeleo la Ubelgiji ENABEL na kituo cha Biashara ITC katika kata ya Choda pamoja ja Irisya ambapo utafanyika uhifadhi wa nyuki na kutoa bidhaa zinazokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi ya Tanzania.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa