Kwa hisani ya ofisi ya mkuu wa wilaya- ya Ikungi
Katika ziara yangu ya kata ya Unyahati kijiji cha mahambe jimbo la Singida mashariki wilaya ya Ikungi, nilitoa mrejesho wa namna gani serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo akiwemo Mhe Mbunge wa jimbo ka Singida mashariki Miraji Mtaturu tulivyotatua changamoto ya maji katika kijiji cha mahambe
Mahembe ni moja katika ya vijiji 8 vilivyopoto kata ya Unyahaati jimbo ka Singida mashariki na changamoto kubwa ilikuwa maji, kwangu sikutaka kuzungumza maneno mengi zaidi ya kwenda kuzindua awamu ya kwanza ya mradi wa maji, kwangu mimi natambua wananchi hawataki hotuba ndefu wala maneno mengi ya michakato wanataka kusikia majibu ya kero na changamoto zao na hapa nikazindua mradi wa maji nikafunga mkutano nikaondoka na kuwaacha wananchi wakifurahi kupata maji safi na salama ya kunywa na shughuli zao zingine
Kwa sasa vijiji vyote nane vinapata huduma ya maji safi na salama, tunachoendelea nacho ni kuongeza wigo (extension) ya miradi yetu ya maji ili iwafikie wananchi wengi zaidi na hatimae kufanikiwa kuwaunganishia maji majumbani mara baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya kupeleka maji kwenye vilula DP,s Domestic Point
Nimefanikiwa pia kuanzisha jumuiya ya watumiaji maji wa kijiji cha mahambe na kuwajengea uwezo wa namna watausimamia na kuendesha mradi huu wa maji kwa kupanga bei za maji, na kukusanya fedha za maji wao wenyewe na kisha kuzielekeza fedha hizo katika kuongeza wigo wa upatikanaji wa maji katika maeneo yao, nimeona nikijenga mfumo imara wa wananchi katika kusimamia maji yao mradi utakuwa endelevu
Asanteni sana wizara ya maji kupitia RUWASA wilaya, asante sana Mhe Miraji Mtaturu Mbunge singida mashariki, asanteni sana wananchi wetu kwa kuwa na subira na sasa kazi imefanikiwa
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa