HAMASHAURI YA WILAYA YA IKUNGI yaendelea na zoezi la chanjo ya mifugo (Ng’ombe) dhidi ya ugonjwa wa upele wa ngozi unaowakabili…
Zoezi hili ni endelevu na linatarajiwa kufanyika katika kata 28 na kufikia sasa tayari kata 16 zimefikiwa na chanjo hiyo inaendelea kutolewa kwenye kata 12 zilizobaki…
Kaimu afisa mifugo wa wilaya Bi Violeth Kidulani amesema kuwa ugonjwa huo unasababishwa na virusi aina ya Neethling Poxvirus na Allerton Herpesvirus ambapo ng’ombe huonyesha dalili za upele mwilini na kutokwa na ute mdomoni….
Aidha kwa upande wao viongozi wavijiji na wafugaji wamepongeza juhudi za serikali kwa chanjo inayotolewa ambayo adhima yake ni kunusuru mifugo katika janga hilo….
Chanjo hii imeanza mwaka 2019 na imefanyika mara tatu mfululizo ikiwa ni kila mwaka mara moja lengo kuu ikiwa ni kutokomeza vifo vya mifugo vitokanavyo na ugonjwa huo.
Ugonjwa wa upele kwa mifugo (Ng’ombe) unaambukizwa kwa njia ya kugusana mnyama moja na mwingine.
(Pichani ni wataalamu wa mifugo kutoka halmashauri ya wilaya ya Ikungi wakiendelea na zoezi la chanjo wakishirikiaa na viongoji wa vijiji.)
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa