Halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida inaendelea kukamilisha zoezi la kuchanja ng`ombe dhidi ya ugonjwa wa mapele Ngozi(lumpy skin disease).
Chanjo hii ni mwendelezo wa kata kumi na mbili zilizobaki ,ata hivyo chanjo hii ilianza kutolewa mwaka 2019 baada ya mlipuko wa ugonjwa huu kutokea katika halmashauri za jirani na wilaya ya Ikungi .
Pia chanjo hii ni zoezi endelevu kila mwaka ili kuendelea kukinga Ng`ombe
dhidi ya ugonjwa huo wa mapele ngozi.
Pichani ni maafisa ugani Ndg Faraji, Elisha Johnson na Grace mweteni wakiwa katika zoezi hilo katika kata ya mang`onyi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa