Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson apokea maagizo ya serikali ya kampeni ya utoaji wa chanjo ya Surua na Rubella katika Wilaya ya Ikungi inayotarajiwa kufanyika Kuanzia tarehe 15 mpaka 18 ya mwezi huu.Hayo yamesemwa leo Tarehe 09 Januari 2024 katika ukumbi wa Halmashauri ambapo katika Kujadili utekelezaji wa maagizo ya serikali ya utoaji wa chanjo ya Surua na Rubella amesema kuwa magonjwa ya Surua na Rubella huenezwa kwa njia ya hewa hususani pale mgonjwa anapokohoa au kupiga chafya na maambukizi huwa ni ya haraka sana hasa sehemu zenye msongamano." Tunalo jukumu kama Wilaya kutoa chanjo hii mapema iwezekanavyo ili kuokoa watoto katika janga hili", amezungumza Mhe ApsonAkisoma taarifa Afisa Afya Wilaya ya Ikungi Ndg Abiudi amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI imeandaa kampeni shirikishi ya kitaifa ya utoaji wa chanjo ya Surua na Rubella ili kuweza kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa Surua na Rubella kwa kuwapatia chanjo hiyo .Afisa Afya ameongeza na kusema kuwa chanjo hiyo itatolewa kwa watoto wa umri wa miezi 9 hadi miezi 59 na jumla ya watoto 55929 wanatarajiwa kufikiwa ndani ya siku 4 katika maeneo yao kama Sokoni, katika ofisi za Serikali, shuleni hasa katika shule za awali na Vituo vyote vya kulelea watoto."Jumla ya timu 80 zimeandaliwa timu hizo zimehusisha watumishi kutoka kwenye vituo vya utoaji wa huduma za chanjo ya kila siku na kila timu itakuwa na watoa huduma watatu ambao ni mchanjaji mmoja, mtunza takwimu mmoja, na mhudumu ngazi ya Jamii mmoja, pamoja na mhamasishaji.Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi amezungumza na kusema kuwa watendaji wa kata na vijiji wanalo jukumu kuhakikisha zoezi hili linaenda sawa kwa kuhakikisha wanafanya uhamasishaji kwa wananchi ili kuhakikisha watoto wote wanapatiwa chanjo kwa wakati kutokana na ratiba ilivyo.Kupitia kikao hiki pia idara ya afya imewasilisha taarifa ya lishe, taarifa ya M-MMAMA, taarifa ya ICHF,pamoja na taarifa ya tamko la jiongeze tuwavushe salama na zote zilijadiliwa na kutoa maadhimia ambayo yanalenga kuimarisha Afya za watanzania hususani katika Wilaya ya Ikungi.Kikao hiki kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi,kamati ya ulinzi na usalama,katibu
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa