Kamati ya fedha na mipango ya wilaya ya Ikungi leo tarehe 3 aprili 2024 amekaa kikao cha robo ya pili kwaajili ya kujadili mapato na matumizi katika kikao hicho Mhe mwenyekiti wa halmashauri Ndg Ally Mwanga amesisitiza kuzingatia vikao vya kisheria vikae kwa wakati kwa kufuata ratiba,kukusanya mapato bila kutosheka na kuendelea kukamilisha miradi ya maendeleo kama standi ya Ikungi,ujenzi wa mnada wa njia panda na kuanzisha mnada kati ya Issuna na Mkiwa kwani mapato mengi yanapotelea Manyoni.Mhe Ilunde wa kata ya Siuyu, pia amesisitiza kujengwa kwa vibanda vya kisasa katika mnada wa njia panda kwaajili ya kupandisha mapato ya halmashauri.Mhe Mwinyi wa kata ya Kituntu nae ameomba kuimalishwa kwa geti ya ukusanyaji wa mapato Utaho na kuwalipa Migambo kwa wakati posho zao.Mwisho Katibu Tawala wa Wilaya Ngd Rashidi Rashidi ameipongeza timu ya mapato kwa usimamizi mnzuri wa ukusanyaji wa mapato kwa kushirikiana na madiwani .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa