Mafunzo ya Jeshi la akiba (Mgambo) yafika tamati Tarehe 10 Novemba 2023 katika viwanja vya Shule ya msingi Ikungi huku mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson.Mhe.Apson amewataka wahitimu wa mafunzo hayo waende kuimarisha ulinzi na Usalama wa wananchi na mali zao na kuwa mfano wa kuigwa na jamii na sio kuwa chanzo cha ukosefu wa amani katika jamii zao.Pia Mgeni Rasmi amewaomba wahitimu hao wa mafunzo kujishughulisha na kazi mbalimbali za maendeleo na kujiajiri pale inapowezekana katika maswala mazima ya ujasiriamali ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.Akisoma Taarifa mbele ya Mgeni Rasmi Lutel Canal Taraya wa Wilaya ya Ikungi amesema mafunzo haya yalifunguliwa mnamo Tarehe 01 July,2023 na Mkuu wa Wilaya Mhe.Thomas Apson kukiwa na washiriki 45 Wanawake nane na Wanaume 37 baadae wakaongezeka kufikia 128 Wanaume 104 na Wanawake 24 na katikati ya mafunzi baadhi yao walipata bahati ya kujiunga na JKT kwa kujitolea kutokana na sifa zao Wavulana wakiwa 12 na Wasichana Sita jumla yao 18 hata hivyo wengine watatu walifukuzwa kutokana na utoro na vijana 9 waliacha mafunzo kwa sababu zao binafsi."Nawapongeza wahitimu wa mafunzo haya kwa kuwa wavumilivu na najivunia kupata Jeshi la akiba vijana shupavu watakao isaidia Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupambana na maswala mbalimbali katika jamii zinazo wazunguka kama vile maswala ya Ruswa,Wizi,Ukatili wa Kijinsia na mambo mengine kadha wa kadha."Amesema Lutel Canal Taraya.MWISHOImetolewa na:Afisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi10/11/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa