Baadhi ya wananchi Wilaya ya Ikungi Kata ya Mgungira kitongiji cha Magungumka wazungumza kero zao moja wapo ikiwa ni pamoja na uhaba wa maji katika eneo hilo hali inayowalazimu kusubiri kwa mda mrefu kutokana na uwepo wa foleni kuteka maji hayo.Wananchi wametaja kero zingine kuwa kuna tatizo la huduma za Afya ubovu barabara kipindi cha mvua ,ukosefu wa umeme na wameongeza na kuomba kugawanyika kwa maeneo ya utawala kati ya Mgungira na Magungumka kutokana na ukubwa wa maeneo uliopo.Hayo yamesemwa Tarehe 01 Novemba 2023 katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi MheThomas Apson Kata ya Mgungira na kuagiza changamoto hizo kufanyiwa kazi kwa wakati ili iweze kuwa msaada kwa wananchi haoAkijibu swali Bwana Victor Afisa kutoka RUWASA Wilaya ya Ikungi mara baada ya kutembelea mradi mpya wa maji unaojengwa katika Kitongoji hicho amesema mradi wa huo wa maji umesanifiwa na kulenga kuhudumia wakazi 5173 wa kitongoji cha Magungumka na kijiji cha Mgungira."Mradi unategemea kugharimu kiasi cha zaidi ya milioni 331.6 mpaka kukamilika kwako"Amesema Bwana VictorMkuu wa Wilaya akiongozana na Afisa Ardhi pamoja na Afisa kutoka RUWASA Wilaya ya Ikungi pia ametembelea ujenzi wa kituo kipya cha polisi Magungumka,mtendaji wa kata amesema Ujenzi umeanza mwaka jana kwa kusaidiana na nguvu za viongozi na wananchi na kufikia sasahivi ni hatua za ukamilishaji na mara baada ya hapo alitembelea Kambi ya wavuvi walioathiriwa na ajali ya moto baada ya kuungua kwa kambi hiyo watu zaidi ya watu 80 wamepata athari na mmoja kufariki dunia papo hapo katika ajali hiyo.Mkuu wa wilaya amesema wapo tayari kutoa msaada kwa walioathiriwa baada ya taratibu kufanyika na kuwashauri kujenga mahema yakudumu yasiyokuwa na hatari tofauti na wanavyojenga kwa kutumia nyasi."Serikali inayoongozwa na mama yetu Dkt Samia Suluhu Hassan inafanya vizuri kwenye miradi mbalimbali kama maji,barabara,umeme,miradi ya shule na maswala ya Afya na tunajitahidi miradi ya namna hiyo iwafikie pia huku."amesema Mkuu wa WilayaMWISHOImetolewa na:Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi01/11/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa