Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson akiongozana na Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Bwana Rashid M.Rashid pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg. Justice L. Kijazi Wafika kujiandikisha kata ya Ikungi kitongoji cha Gahilu katika kituo cha kujiandikishia uchaguzi wa serikali za mitaa.
Zoezi hilo la uandikishaji limeanza leo tarehe 11 Octoba, 2024 Rasmi Saa mbili za asubuhi na litadumu kwa siku kumi mpaka tarehe 20 Octoba, 2024 ambapo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi amehamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi ili wajiandikishe kwani ni haki yao ya msingi.
Mkurugenzi Mtendaji ameongeza na kusema kuwa kila kitongoji kina kituo Rasmi cha kujiandikisha na wananchi wenye umri kuanzia miaka 18 wana haki ya kwenda katika vituo hivyo kujiandikisha na baadae majina yatabandikwa kwenye vituo hivyo kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Bwana Rashid M.Rashid amewaomba waendeshaji wa zoezi hilo kote Wilaya ya Ikungi kuwapa kipaumbele watu wenye ulemavu, kinamama wajawazito, pamoja na wazee ili wapate huduma mapema na kurejea majumbani kwao.Kauli mbiu ya uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024 ni "Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki uchaguzi" #uchaguziwaserikalizamitaa#nitashiriki
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa