Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Thomas Apson awataka wauguzi kuwa na kauli nzuri kwa wagonjwa katika Hospitali, vituo vya afya pamoja na Zahanati kwani hali hiyo inashusha sifa ya Wilaya na hata kuongezeka kwa vifo pale wagonjwa wasipohudumiwa ipasavyo.Hayo yamesemwa hii leo terehe 28 katika kikao cha kawaida cha Tujiongeze tuwavushe salama, M-MAMA, Lishe, ICHF cha tarehe 28 Mei, 2024 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.Mkuu wa Wilaya amesema kuwa changamoto ya kauli mbaya kwa wagonjwa imesemwa mara kadhaa katika Tarafa ya Sepuka na kumwomba Afisa Ustawi wa jamii kufuatilia kwa karibu swala hilo na kuwachukulia hatua wauguzi wanaoenda kinyume na taratibu za kazi.Aidha katika kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi Haika Massawe, Mganga Mkuu wa Wilaya , Watendaji wa kata pamoja na waganga wafawidhi wa Hospitali, Zahanati na vituo vyote vya afya Wilaya ya Ikungi ajenda mbalimbali zimejadiliwa.Katika kikao hicho zimesomwa na kujadiliwa taarifa za lishe, taarifa za afya ya Uzazi na Mtoto, taarifa ya M-Mama pamoja na taarifa ya mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa ICHF na mengineyo ambayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji amesema tunapaswa kuyapa kipaumbele ili kuboresha afya kwa wananchi wa Wilaya ya IkungiMwisho Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Dkt Dorisila John ameongeza na kusema kuwa kila kituo kinapaswa kuhamasisha wananchi kujiunga na pia kuhimiza wanafunzi katika shule zote wajiunge na mfuko wa bima ya afya ya jamii"Na pia kutoa elimu ya Afya ya uzazi kwenye mikutano ya hadhara na kwa wasichana walioko shule na nyumbani" amezungumza Mganga Mkuu
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa