Mkuu mpya wa Wilaya ya Ikungi Mh. Jerry Cornel Muro amefanya ziara yake ya kwanza kwa kuzungumza na watumishi mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi.
Ziara hio kwa watumishi imefanyika leo tarehe 22/06/2021 ambapo alikuwa ameongozana na Katibu tawala ndugu Winfrida Funto, Afisa usalama wa wilaya , afisa TAKUKURU wa wilaya na baadhi ya maafisa wa kamati ya ulinzi na usalama.
Mh. Muro ametoa shukrani kwa kuweza kuaminiwa na Mh. Rais ya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kumteua kuiongoza wilaya ya Ikungi. Pia ametoa pongezi kwa wilaya ya Ikungi kwa kuweza kupata hati safi mara saba mfululizo.
Alisisitiza halmashauri lazima iwe na vipaumbele ambavyo vitaweza kuifanya halmashauri ifanye vizuri zaidi. Baadhi ya Vipaumbele alivyosisitiza ni kuwa na "BRANDY'' alisema " ili Wilaya iweze kutambulika inatakiwa ijiwekee brandy yake ambayo ni tofauti na mahali pengine popote" alitolea mfano kilimo cha Alizeti kama zao la wilaya, ambapo kama wilaya itawekeza kwenye kilimo cha alizeti itapata faida kubwa na kujulikana zaidi.
Pia amesisitiza katika uongozi wake atahakikisha kupunguza ziro katika shule zote za sekondari ili wilaya iweze kufanya vizuri kielimu. Jukumu kuimarisha ulinzi na usalama katika wilaya ili wakazi wa Iikungi waweze kufanya kazi zao kwa uhuru na amani.
Mikakati mingine aliyoipa kipaumbele ni kuhakikisha halmashauri inabuni vyanzo vipya vya mapato kwa kuweka sera nzuri za kuvutia wawekezaji. Ametolea mfano wa kuwashawishi wawekezaji wa vituo vya kuuza mafuta ''Halmashauri itapata service levy kubwa kwa wafanyabiashara wa mafuta kuliko kung'ang'ania ushuru wa wajasiliamali wadogo''
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa