Maneno hayo yamezungumzwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro amewahakikishia wananchi kuwa ujenzi wa vyumba vipya 67 vya madarasa ya shule za sekondair na vyumba vipya 63 vya madarasa ya shule shikizi za msingi yatakamilika ndani ya muda uliopangwa
DC Muro akitoa taarifa ya awamu ya kwanza ya kutembelea na kukagua kazi ya ujenzi wa madarasa 130 yanayojengewa wilaya ya Ikungi yenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 amesema wao wamejipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri ya haraka katika ujenzi wa madarasa, ambapo amemshukuru Mhe, Rais. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia wilaya hiyo kupewa mgao mkubwa wa fedha .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa