Mkuu wa Mkoa hapa Singida, Dkt. Bilinith Satano Mahenge, amefanya ziara ya kutembelea wilaya Ikungi . Katika ziara hio amembatana na Katibu Tawala wa mkoa pamoja na maafisa mbalimbali. Mahenge ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Ikungi kwa kufanya vizuri na kushika nafasi ya kwanza kimkoa katika ukusanyaji wa mapato.
Amesisitiza ili Halmashauri ifanye vizuri katika ukusanyaji wa mapato, haina budi kila idara na kitengo kiweze kusimamia mapato , na si jambo la idara ya Fedha peke yake.
Ametoa mfano maafisa kilimo na mifugo wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kusimamia mapato hayo kwani kwa kiasi kikubwa mapato mengi yanatoka katika idara zao.
Hata hivyo ameonesha kutoridhishwa na mwenendo wa ukusanyaji wa mapato kwani wafanyabiashara na baadhi ya maafisa wa kukusanya mapato hawatimizi wajibu wao. halmashauri '‘matapo mengi yanapotea kutokana na kukosa usimamizi bora hali hii inayopelekea upotevu mapato ya serikali.’'
Amewahimiza watumishi wawe makini na kuzingatia karatibu na miongozo ya afya kuhusu kujikianga na ugojwa wa UVIKO-19. Amesema ''ugonjwa huu upo na tunatakiwa tujitokeze kwa wingi kupata chanjo na kuzingatia taratibu zote za afya '' Mpaka kufikia jana tarehe 10 takwimu zinaonyesha wilaya ya Ikungi imechanja watu 253 tu na kimkoa watu 2484.
Katika Ziara hio Mkuu wa mkoa pamoja na timu yake walitembelea jengo jipya la hospitali ya wilaya pamoja na jengo la VETA ili kuweza kuona maendeleo ya ujenzi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa