Kamati ya kudhibiti ukimwi halmashauri ya wilaya ya Ikungi imekaa leo 23 octoba 2023 katika kikao cha kawaida na kujadili shughuli zilizotekelezwa katika robo ya kwanza julai mpaka septemba .Katika kikao hicho Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti Ukimwi Mhe Mtyana S. Petro amesema kuwa katika vikao hivyo uko kwenye kata waheshimiwa Madiwani washirikishwe ili kuhamasisha jamii zaidi na kupata uelewa juu ya elimu ya kudhibiti Ukimwi .Pia katika kikao hicho Katibu wa kamati ya kudhibiti Ukimwi Ndg Peter Nchembi ameongeza kwa kusema kuwa elimu hii ya kudhibiti Ukimwi ni endelevu na tunazidi kuitoa kwa jamii kwa kupita kila kata na kuhakikisha kila mtu inamfikia ili kupungua kiwango kikubwa cha maambukizi .Pia Mratibu wa kuthibiti Ukimwi Ndg Yesaya Mawazo amesema kuwa kwa sasa maambukizi kwa robo ya kwanza julai -septemba ni asilimia 1.5 ambapo wanaume 15,877 wamepima na waliopata maambukizi VVU ni 117 na wanawake 9011 wamepima na waliopatikana na maambukizi ya VVU ni 128.Pia ameongeza kwa kusema kuwa elimu imezidi kutolewa kwa jamii kwa kutoa ushauri nasaha, upimaji na tiba na umuhimu wa upimaji wa VVU pamoja na matumizi sahihi ya Kondomu kwa waliokutwa na maambukizi ya VVU kwa robo ya kwanza .Pia amesisitiza kuwa wakati wa kutoa elimu kwa jamii tuwe na usiri na upendo kwa waathirika pamoja na kuwa mabalozi kwa ngazi ya famila ili kubadili tabia za watoto wetu.Mwisho Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe Aliy J Mwanga amesema kuwa jukumu ili la kuelimisha jamii ni letu sote haswa sehemu za ibada na mikusanyiko ya watu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa