Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe.Thomas Apson afanya mkutano na wadau wa mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani Wilaya ya Ikungi lengo ni wadau hao kujua namna ya kusimamia mfumo huo unaolenga kuwanufaisha wananchi kiuchumi.
Hayo yamefanyika hii leo tarehe 09 Julai, 2025 katika ukumbi wa Halmashari ya Wilaya ya Ikungi ambapo DC Apson amewataka wakulima kutumia mfumo huu ili kukuza uchumi wao.
DC Apson ameongeza na kusema kuwa kuna haja ya kutoa elimu yakutosha kwa wakulima, kutambua maeneo yasiyokuwa na maghala ili mikakati ifanyike kujengwa kwa maghala hayo na kuhamasisha wakulima kufungua akaunti za benki ili kurahisisha malipo kwa wakulima.
Akisoma taarifa ya usimamizi wa mfumo wa stakabadhi ghalani kwa msimu wa mwaka 2024/2025 Afisa Kilimo Ndg. Issa Mtweve amesema kuwa Ikungi imeanza kutekeleza mfumo huu rasmi mnamo tarehe 17 Agosti, 2024 baada ya kufanya mikutano ya uhamasishaji na uhabarisho katika maeneo yanayolima mazao ya jamii ya kunde na ufuta.
Katika msimu wa kilimo 2024/2025 jumla ya kilogram 785,056 zilikusanywa na kuvuka malengo ya 654,000 sawa na asilimia 120 ya lengo la makusanyo yote ya mazao haya, hiyo ni dalili njema kuwa mfumo huu umefanikiwa kwa kiwango kikubwa" ameeleza Afisa Kilimo
Baadhi ya wajumbe wa vyama vya ushirika wametoa maoni yao katika kikao hicho na kusema kuwa Halmashari itengeneze mikakati madhubuti kudhibiti utoroshaji wa mazao nyakati za usiku katika maeneo ya Mungaa pamoja na Mkiwa ili kuongeza mapato katika Halmshauri ya Wilaya ya Ikungi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa