Elimu ya Urasimishaji Biashara na huduma zitolewazo na Taasisi za kifedha kwa Wanawake huku wanaume nao wakishiriki zatolewa kuwezesha kukuza uchumi Wilaya ya Ikungi.Afisa Biashara Bi Diana Kashaija wakishirikiana na TCB Bank pamoja na Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi wamefanya uhamasishaji wa kukuza na kuendeleza biashara katika kata ya Ikungi Kijiji cha Matongo Tarehe 16 Novemba 2023.Aidha Afisa Biashara Amewashauri wafanya biashara kuweka akiba na kuchukua mikopo isiyoumiza kwenye Taasisi za kifedha ili kukuza biashara zao.Kwa upande wake Afisa Maendeleo Bwana Peter Mussa Nchembi amewahimiza wanawake kuwa na utamaduni wa kuweka akiba na ufanyaji biashara kwa tija ili kuwainua kiuchumi.MWISHOImetolewa na;Afisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi16/11/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa