Wachungaji na mashehe waaswa kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto hapo jana 15 januari 2024. Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi Ndg Antony Mwangolombe amesema wachungaji na mashehe watusaidie kutoa elimu hii ya ukatili wa kijinsia katika makanisa na misikiti kwani huko ndiko kuna mkusanyiko mkubwa wa watu.Pia ameongeza kwa kusema wazazi tubadilike katika malezi ya vijana wetu ,kijana wa kiume afanye kazi sawa na kijana wa kike pasiwe na mipaka katika shughuli mbalimbali katika jamii. Mjumbe wa kamati ya MTAKUWWA Ndg Chima ameongeza kwa kusema elimu hii ya ukatili itolewe pia kwa wanaume kwani kuna wanaume wanafanyiwa ukatili na wanashindwa kutoa taarifa zao sehemu husika kama police na kitengo cha ustawi wa jamii. Nae Mchungaji wa kanisani la Luthelani wilaya ya Ikungi , ameahidi kuongeza kitengo cha kuelimisha jamii kuhusu ukatili wa kijinsia dhidi wanawake, watoto pamoja na wanaume hapo kanisani.Ndg Yesaya Mawazo kutoka Idara ya Afya amesema kuwa ili tuwe na usawa jamii kwanza itazame chanzo cha hayo yote kwanini yanatokea katika jamii,itazame malezi ,mila na desturi zetu hapo mwanzo zilikuwaje ,ametolea mfano wa utoaji mali ,kwanini kijana wa kiume atoe mali,kwanini wasioane bila mali ili kuweka usawa. Mwisho
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa