EQUIP- T Ni Mpango wa kuboresha elimu unaofadhiliwa na na serikali ya Uingereza kupitia ofisi ya Rais TAMISEMI. Kupitia mpango huo,
Halmashauri ya wilaya ya Ikungi imeweza kupata ufadhili huo kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vyumba vya madarasa na ofisi za waalimu.
Miradi ya EQUIP-T iliyopata fedha ya mwaka 2018/2019 ni shule shikizi ya Kaugeri, shule shikizi Mwale na na umalizaji wa boma wa shule ya msingi darajani zote zikiwa ni jumlaya Tsh 145,200,000
Mraratibu wa EQUIP-T Wilaya ya Ikungi ndugu Imani Maketa ametaja fedha zilitolewa na matumizi yake kwa shule husika.
Shule shikizi ya Kaugeri iliyopo tarafa ya Mwaru ambayo imepatiwa Tsh milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa, Ofisi moja ya waalimu na matundu 6 vya vyoo.
Aliyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na kamati ya ujenzi ya shule ya msingi Kaugeri.
Pia Shule ya msingi Mwale iliyopo tarafa ya Iglansoni nayo imepatiwa Kiasi cha tsh milioni 60
kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa, ofisi moja ya waalimu na matundu 6 vya vyoo.
aliendelea kusema Shule ya msingi Mwale iliyopo tarafa ya Mkiwa imepatiwa shilingi 25,200,000 kwa ajili ya ukarabati wa Madarsa mawili na ofisi ya waalimu.
Naye Afisa Elimu msingi Wilaya ya Ikungi ndugu Gidion Kitoboli aliisisitiza kamati ya ujenzi yan shule ya Kaugeri Kufanya kazi ya kamati kwa ueledi na kujituma. pia amesisitiza pindi fundi atakayeshinda zabuni kupatiakana,
Kamati inunue vifaa na kuanza kazi mara moja.
" Pesa ipo tayari kwenye akaunti za shule husika hivyo basi naitaka kamati itakapompata fundi inunue vifaa vyote vinavyohitajika na ujenzi uanze mara moja"
Kamati ya ujenzi wa shule ya msingi kaugeri wakisililiza maelekezo toka kwa afisa elimu ndugu GIDIONI pamoja na timu yake ya Halmashauri
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa