Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi apokea wageni kutoka Ethiopia Wizara ya Kilimo kujifunza kuhusu kilimo hai cha pamba wilayani Ikungi.
Akizungumza nao ofisini kwake leo Tarehe 28 Agosti,2023 kabla ya kutembelea vijiji wanavyolima pamba Wilayani hapa Mkurugenzi amesema kuwa Kilimo cha pamba ni kilimo kinachokuja kwa kasi Wilaya ya Ikungi hii ni kutokana na ubora wa ardhi kwa ajili ya kilimo hicho.
"Hivyo naamini mtajifunza na kushirikiana nasi pale itakapohitajika ili tuweze kujifunza pia kutoka kwenu" Alisema Kijazi
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Ikungi Rashid Rashid amewapongeza kwanza kuichagua Ikungi kama eneo lao la kujifunza na hatimaye kushirikiana mara baada ya kujifunza kutoka Ikungi.
Afisa Kilimo Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Gurisha Msemo amesema kuwa Kilimo cha Pamba kinafanyika katika kata mbalimbali kama vile Makilawa,Minyughe,Kikio,Misughaa,Makiungu,Siuyu,Mng'onyi,Mwaru,Iglansoni,Mtunduru,pamoja na Ighombwe ambapo pamba hiyo inazalishwa na kupelekwa kiwandani kwa ajili ya kuchakatwa.
Ndg Msemo ameongeza na kusema kuwa wakulima wote wamepata mafunzo ya uzalishaji na hatua zote hadi kufikia mavuno wanatumia njia za asili mfano uwekaji wa mbolea,dawa za kudhibiti wadudu waharibifu na dawa za kuhifadhi Pamba hiyo.
"Hivyo nawakaribisha wote wanaotamani kujifunza Kilimo Hai Wilayani kwetu hatimaye kukuza sekta ya Kilimo Nchini"Amezunguza Afisa Kilimo
Aidha Afisa Kilimo ameipongeza Bodi ya Pamba kwa ushirikiano wanaouonesha Hali inayopelekea uzalishaji kuongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa msimu wa 2022/23 uzalishaji ulikuwa Kilogramu 564,774 lakini kwa msimu huu ni 973,567 na msimu wa manunuzi bado uko nusu sasa.
Pia aliendelea kuishukuru Kampuni ya Biosustain Tanzania Limited ambayo ndio Kampuni kuu inayosaidia uzalishaji na ununuzi kwa kuwa mstari wa mbele katika zoezi la kuongeza uzalishaji na kutoa bei nzuri kwa wakulima na kwa wakati.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa