Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Azindua Gari la Kikundi cha Ufyatuaji Tofali "Tujitume"
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mhe. Ally J. Mwanga, leo tarehe 14 Februari 2025, amezindua gari la kikundi cha ufyatuaji tofali "Tujitume" lenye thamani ya shilingi milioni 80. Gari hilo litatumika katika shughuli mbalimbali za kikundi hicho.
Akizungumza wakati wa uzinduzi uliofanyika katika Kata ya Ikungi, Mhe. Mwanga amewasihi wanachama wa kikundi kujituma kwa bidii na kuhakikisha wanarejesha mikopo waliyopewa kwa wakati.
Kikundi cha "Jitume Vijana" kilianzishwa rasmi mwezi Septemba 2019 na kikasajiliwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi tarehe 7 Oktoba 2019 kwa namba ya usajili IDC/CSO/970. Kikundi kilianza kikiwa na wanachama 10, wakiwemo wanaume saba (7) na wanawake watatu (3), wenye umri wa miaka 18-35.
Aidha, kikundi hicho kilipata usajili mpya kwa njia ya mfumo wa kisasa tarehe 29 Oktoba 2024 kwa namba SIN/IKU/VIJ/2024/0029. Kwa sasa, kina wanachama watano (5), wakiwemo wanaume watatu (3) na wanawake wawili (2), wenye umri wa miaka 18-45
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa