Kikao cha makubaliano hayo kimefanyika leo 4/5/2021 baina ya wawakilishi kutoka Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi stadi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Uongozi wa VETA mkoa wa Singida Pamoja na Mkuu wa wilaya ya Ikungi Mh. Edward Mpogolo.
Kupitia barua yake yenye kumb Na. BC. 361/386/01A/08 ya tarehe 06 Februari 2021 Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi stadi iliagiza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kufanya tathmini ya kazi zilizokwishafanyika na Kukabidhi Mradi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi ili iweze kukamilisha sehemu ya mradi iliyosalia.
Mradi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi stadi Wilaya ya Ikungi, upo katika Kata ya Ulyampiti, Kijiji cha Muungano, Kilomita 6 kutoka makao makuu ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida.
Eneo la mradi lina ukubwa mita za mraba elfu ishirini na mbili na mia mbili hamsini ( 22,250 sqm).
HABARI PICHA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndugu Justice Kijazi na Mh. Edward Mpogolo wakiweka sahihi makubaliano ya awali ya makabidhiano ya mradi.
Viongozi toka Wizara Ya Elimu, Sayansi Na Teknolojia wakiweka sahihi makubaliano ya mkataba
Kaimu mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Ikungi akisoma mkataba huo kabla ya kusainiwa
Wakuu wa Idara na vitengo wakisikiliza kwa makini mjadala
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa