Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi imekutana na kujadili taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi kilichoishia Mei 31, 2025, ambapo zaidi ya shilingi bilioni 3.4 zimekusanywa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 16 Juni, 2025 katika ukumbi wa halmashauri, kikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Mhe. Ally J. Mwanga.
Mbali na taarifa hiyo, ajenda nyingine zilizojadiliwa ni pamoja na taarifa ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri (awamu ya tatu), pamoja na taarifa ya makabidhiano ya miradi ya uwajibikaji kwa jamii (CSR) iliyotekelezwa na Shanta gold mining.
Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mwanga amesema kuwa timu ya ukusanyaji mapato inapaswa kuboreshwa zaidi ili kuongeza ufanisi wa kazi na kufikia lengo la halmashauri la kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 7 kwa mwaka.
“wakusanya mapato wanapaswa kudhibiti mianya ya utoroshaji wa mapato ya mazao kwa kuzuia mapato hayo kulipwa katika halmashauri nyingine za jirani, mikakati iandaliwe na timu ya mapato iongeze ubunifu wa kukusanya mapato ili tuweze kufikia malengo ya kukusanya shilingi billion sabaalisema Mhe. Mwanga.
Aidha, ameipongeza halmashauri ya wilaya ya Ikungi kwa kuendelea kupata hati safi kwa kipindi cha miaka 10 mfululizo, akisema kuwa mafanikio hayo ni uthibitisho wa uwepo wa uongozi bora na usimamizi mzuri wa fedha za umma ndani ya halmashauri hiyo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa