Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi yakabidhi hundi ya zaidi ya milioni 278.2 kwa vikundi 17 mkopo wa asilimia 10 wa wanawake,vijana na walemavu, hatua Kali kuchukuliwa kwa watakaoenda kinyume na makubaliano yaliyowekwa dhidi ya mkopo huo.
Hayo yamesemwa hii leo tarehe 20 Disemba 2024 katika ukumbi wa Halmashauri na Mhe Ally Mwanga akimuwakilisha Mbunge wa jimbo la Singida mangharibi Mhe Elibariki Kingu kuwa kumeibuka tabia ya vikundi kubadili matumizi ya fedha za mikopo na wengine kukimbia na fedha hizo.
"Hatua Kali za kisheria zitachukuliwa kwa wote watakaofanya hivyo" amesema Mwanga.
Mkurugenzi Mtendaji Ndg Justice Kijazi akisoma taarifa amesema kuwa halmashauri ya wilaya ya Ikungi tayari ilikuwa imeshatoa mikopo yenye thamani ya milioni 852.1kwa vikundi 271 vya wanake vijana na watu wenye ulemavu ambapo kati ya fedha hizo vikundi 186 vya wanawake vilipatiwa mikopo yenye thamani ya milioni 476.9, vikundi vya vijana 58 mikopo ya Shilingi 303.2 na vikundi vya watu wenye ulemavu 27 mikopo ya milioni 71.9 na kupekekea jumla ya wanufaika 1870 walipata mikopo hiyo iliyowawezesha kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi, ufugaji , kilimo biashara ndogondogo na Tehama.
Kijazi ametaja changamoto zilizopo katika utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kuwa ni pamoja na baadhi ya vikundi kutorejesha mikopo kwa wakati, vikundi kubadili matumizi ya fedha walizokopeshwa hata kabla ya kutekeleza miradi waliyoombea fedha, mabadiliko ya hali ya hewa kuathiri miradi ya Kilimo,uhaba na bei kubwa kwa baadhi ya malighafi za miradi hivyo kukwamisha uendelevu wa miradi
Kukosekana kwa mtandao wa usajili kwenye baadhi ya maeneo,uhaba wa vitendea kazi kwa wataalam wanaoratibu mikopo hii hususan usafiri, vifaa vya kusajilia vikundi kwa njia ya kielektroniki laptop na vishkwambi na vifaa vya hamasa kama vile vipaza sauti na kutokuwepo kwa mafunzo ya kina kwa vikundi.
"Kwa niaba ya wananchi wa Ikungi naishukuru Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Mhe.Rais Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa mikopo hii kwa wananchi na kuridhia ianze kutolewa tena baada ya kuboreshwa taratibu wa utoaji na usimamizi wa mikopo hii" amesema Kijazi
Kwa upande wao baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo wameishukuru serikali kwa kushirikiana vyema na Halmashauri ya wilaya ya Ikungi kurejesha mikopo hiyo kwani imekuwa msaada kuinuka kiuchumi hususani wanawake, vijana na watu wenye mahitaji maalimu.
Halmashauri kwa kuzingatia kifungu 8(1) cha Kanuni za utoaji na usimamizi wa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu za mwaka 2024 ilitangaza kufunguliwa kwa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na uwepo wa fedha kiasi cha Shilingi milioni 595 kwa uwiano wa 4:4:0
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa