Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Yatekeleza Bajeti ya Shilingi Bilioni 47 kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026
Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, mkoani Singida, imepanga kukusanya na kutumia jumla ya shilingi 47,415,676,858 kwa mwaka wa fedha wa 2025/2026.
Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Kastoli George Msigala, wakati wa kuwasilisha mpango na bajeti ya mwaka husika kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Msigala, kati ya kiasi hicho, vyanzo vya mapato na matumizi vimegawanyika kama ifuatavyo:
• Mapato ya ndani: Shilingi 5,051,412
• Ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa miradi ya maendeleo: Shilingi 4,668,366,221
• Ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa matumizi mengineyo (OC): Shilingi 2,798,637
• Wahisani: Shilingi 5,564,259
• Mishahara: Shilingi 29,347,048,750
Msigala alieleza kuwa mapato ya ndani ya halmashauri yamegawanywa katika maeneo mawili makuu, ambayo ni mapato huru na mapato fungwa.
“Kwa upande wa mapato huru, mgawanyo wake unahusisha maeneo matatu: asilimia 10 kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu; asilimia 30 kwa ajili ya miradi ya maendeleo; na asilimia 60 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, yakiwemo matumizi ya uendeshaji wa ofisi,” alifafanua Mkurugenzi Msigala.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa