Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mh. Mtaturu awataka wananchi ambao hawakupanda mikorosho waweze kupanda zao hilo huku akiwahakikishia kuwa miche ipo ya kutosha.
Alisema kama wilaya imejiwekea mikakati ikiwemo kuwa na eneo maalum litakalotumika kama shamba darasa kwa ajili ya zao hilo lengo likiwa baada ya miaka mitatu kuwe na uchumi mkubwa wa korosho.
“Tumetenga eneo katika kijiji cha Mkiwa heka mia tano kwa ajili ya upandaji wa mfano,tayari kijiji kimeridhia hivyo kwa sasa tunaweka utaratibu wa watu kupata maeneo yao ili wakapande mikorosho kwa wingi,”alisema Mtaturu.
Aliongeza kuwa miche ipo na inatolewa bure hivyo watumie vizuri mvua zinazoendelea kunyesha kwa ajili ya kupanda.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa