Madiwani Pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida wafanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi ili kupata mafunzo kuhusu Hewa ya ukaa na namna ya kuongeza mapato ya Halmashauri kupitia utunzaji wa misitu.Mafunzo hayo yameanza leo Tarehe 14 Agosti,2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika yakifatiwa na kutembelea misitu hiyo hapo kesho na kujifunza namna wananchi na uongozi wa vijiji pamoja na Halmashauri wanavyoshirikiana katika utunzaji wa Misiti hiyo.Aidha Wilaya ya Ikugi imedhamiria kuanzisha kampeni ya upandaji miti pamoja na kuboresha mazingira yake kwa ujumla,Dhamira hii imetokana na matakwa ya sheria ya Taifa ya misitu namba 14 ya mwaka 2002 inayosistiza kuhusu jamii zinazoishi karibu na hifadhi za misitu, kumiliki, kusimamia na kunufaika na utumiaji endelevu wa rasilimali za misitu kutoka ndani ya hifadhi hizo. Sheria inaruhusu jamii kugawana faida zinazotokana na usimamizi wa pamoja wa misitu inayomilikiwa na serikali kuu. Pia sheria ya misitu na. 14 ya mwaka 2002 inatoa mamlaka kwa serikali ya kijiji (kupitia kamati ya kijiji iliyoteuliwa) kuanzisha hifadhi ya misitu kwenye ardhi ya kijiji na kutoa vibali vya kuvuna mazao ya misitu kutoka kwenye hifadhi za misitu ya kijiji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani au kibiashara ( kifungu 49 (6). Mkuu wa Msafara Bi Haika Massawe akimuwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ndg Justice Kijazi amesema kuwa lengo la ziara hii ya mafunzo wilayani Tanganyika ni kujifunza namna wenzetu walivyofanikiwa kusimamia na kutunza mazingira (misitu) kwa kuangalia namna uhifadhi wa mazingira (upandaji wa misitu) unavyofanyika, usimamizi wake na uvunaji wa rasilimali zake, faida zilizopatikana kutokana na misitu (uhifadhi wa mazigira) pamoja na mahusiano ya kisera, kisheria na miongozo na shughuli za uhifadhi zinazofanywa na Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika. "Mwisho ni kujifunza changamoto ambazo Halmashauri imepata kupitia shughuli za uhifadhi na utatuzi wake kama upo."amesema Bi Haika Masawe.MWISHOAfisa Habari Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi 14/08/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa