Mwenyekiti wa Halmashsuri ya Wilaya ya Ikungi Mhe. Ally J. Mwanga awaomba madereva wa Huduma ya Usafiri kwa mama wajawazito, wenye Uchungu, waliojifungua pamoja na watoto wachanga M-MAMA kuzingatia mafunzo watakayopewa ikiwemo swala la usiri katika kazi zao.Hayo yamesemwa leo Tarehe 09 Agosti 2023 katika ufunguzi wa mafunzo maalumu kwa madereva hao ukumbi wa Halmashsuri ya Wilaya ya Ikungi ambapo Mwenyekiti amesema mafunzo yanayotolewa ni mahususi kwa ajili ya kumjenga dereva awe na uwezo wa kukabiliana na shughuli hiyo ya usafirishaji nyakati zote wanapohitajika."Tofauti na Madaktari huwa wanakula kiapo kutunza siri nyie ni madereva mnaokwenda kutoa msaada kwenye jamii zetu tuwe wasiri sana"alisema Mhe.Mwanga.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Bi-Haika Massawe ameongeza na kusema kuwa Halmashsuri itatoa ushirikiano kwa madereva na amewaomba viongozi wa Afya kuwapa ushirikiano madereva hao pia ili huduma hiyo iwe msaada kwa Jamii.M-mama mfumo wa usafirishaji wa dharura ulioboreshwa kwa Mama wajawazito,walioko kwenye uchungu,na waliojifungua hadi siku 42 pamoja na watoto wachanga.Mganga Mkuu Wilaya ya Ikungi amesema kuwa lengo la huduma hii ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto wachanga.Huduma hii inatumia magari ya kusafirishia wagonjwa (Ambulance) pamoja na magari ya madereva ngazi ya jamii ambao leo hii wanapatiwa mafunzo maalumu na kusaini hati ya makubaliano na Halmashauri kama usafiri wa dharura kutoa huduma hiyo.MWISHOAfisa HabariHalmashauri ya Wilaya ya Ikungi09/08/2023
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa