Idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Ikungi yatoa mafunzo kwa wanawake kata ya Mungaa pamoja na Minyughe ili kuwajenge uwezo wanawake juu ya maswala ya uongozi na haki ya umiliki wa mali kupitia mradi wa WILA.
Mradi wa WILA ni mradi unaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la UNWOMEN ambalo linafanya mradi huo katika wilaya tatu mkoani singida na katika wilaya ya Ikungi mradi huo unafanyika katika kata mbili ambazo ni Mungaa Pamoja na Minyughe.
Hayo yamefanyika hii leo tarehe 24, octoba 2024 katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida ambapo wanawake zaidi ya 70 wamepata mafunzo hayo ambayo yanalengo la kumuwezesha mwanamke kiuchumi na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili hasa kutoa maamuzi kwenye uongozi pamoja na haki ya kumiliki mali.
Hata hivyo mafunzo yameambatana na maelekezo ya namna ya kuomba mkopo wa asilimia kumi za halmashauri ambao moja ya walengwa ni pamoja na wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ambapo afisa maendeleo halmashauri Ndg. Peter Nchimbi akishirikiana na Mariam Mwandikile amesema mambo muhimu ambayo walengwa wanapaswa kuwa nayo ni pamoja na kuunda vikundi na kupata maelekezo juu ya kujisajili kwenye mfumo, kitambulisho cha nida au namba ya nid, kutengeneza katiba na mambo mengine ambayo amesema walengwa watapatiwa elimu kabla ya kuchukua mkopo huo.
"Mkufunzi amefundisha kuhusu sifa za uongozi, aina za viongozi faida za ushiriki wa wanawake katika uongozi ambapo amesema kuwa katika ya ibara ya 12 ya katiba inasema kuwa binadamu wote ni sawa na huzaliwa huru hivyo wote tupo sawa katika kila jambo hasa kwa upande wa mwanamke na uongozi hivyo ni lazima kuzingatia hayo” amezungumza Mariam Mwandikile
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa