Afisa Kilimo wa Halmashauru ya Wilaya ya Ikungi Gurisha Msemo athibitisha kupokea Tani 25 za Mbegu ya Alizeti tarehe 01 Desemba 2022 katika ghala la wilaya ya Ikungi itakayo wanufaisha wananchi wa eneo hilo.
Akizungumza alipokuwa akitoa taarifa mbele ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Jerry Muro Gurisha amesema kuwa kutokana na upungufu wa mbegu bora waliadhimia kuomba kupitia mkuu wa mkoa wa Singida Ndg Peter Serukamba na hatimaye mbegu zimewafikia.
"Kiasi cha mbegu tulichoomba ni Tani 150 lakini Wizara kupitia ASA tumepata Mgawo wa tani 92 na mbegu tulizoanza kupokea ni tani 25 aina ya Record C1.Ni mbegu bora na Imethibitishwa na maalaka ya Uthibiti wa Mbegu Tanzania."Alisema Gurisha.
Pia ameongeza na kusema kuwa Wamepokea mbole tani 30 aina ya DAP kati ya tani 250 za mahitaji yetu kutuka TFRA mzalishaji ni EGT na wakala wa kusambaza ni Singidani Agro Diller.
Aidha alisema hiyo Mbegu itauzwa kwa bei ya Tshs 5,000 kwa kilo na Kg 2 itakuwa elfu 10,000 pia mbolea itauzwa kwa Tshs 70,000.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Mhe Jerry Muro Pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Ally J. Mwanga wameishukuru serikali kwa kusikia kilio cha wananchi wa Ikungi na kuomba wananchi kununua kwa wingi mbegu hiyo na mbolea ili kuwahi msimu wa kilimo.
Tazama habari picha
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa