Kwa hisani ya ofisi ya mkuu wa wilaya Ikungi.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi Ndugu Jerry C. Muro amewaomba wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi katika maeneo amabyo miradi ya ujenzi wa madarasa unaendelea
Dc Muro ametoa wito huo wakati akitoa taarifa ya ujenzi pamoja na kuwataka wananchi wa ikungi kuchangamkia fursa za ujenzi, usambazaji wa vifaa vya ujenzi na kuwataka wananchi kuhakikisha wanatumia vizuri fursa ya miradi ya ujenzi kujipatia kipato halali kwa kufanya kazi
Dc Muro amesema wilaya ya Ikungi imepewa shilingi Bilioni 2.6 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vipya 67 vya madara ya sekondari na ujenzi wa vyumba vipya vya madarasa 63 ya shule shikizi za msingi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
Anuani ya Posta: S.L.P 42, Singida, Tanzania
Simu ya mezani: +255262964037/6
Mobile:
Barua pepe: ded.ikungidc@singida.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi. Haki zote zimehifadhiwa